LIUMAHABARI BLOG
Monday 13 March 2017
Friday 7 October 2016
MISINGI YA KUIFAHAMU KABLA HUJAANZA BIASHARA.
karibu sana mpenzi msomaji wetu wa mtandao wa DUNIA MPYA mtandao unaokupa habari matomoto za kukuburudisha na kukuelimisha, Katika mada yetu ya leo nimekuletea misingi ya kuifahamu kabla hujaaanza biashara yeyote ile.... Ukweli ni kwamba hakuna mtu apendae kuanza biashara yake harafu punde kuiona biashara hiyo ikiishia sehemu ambayo hakuitarajia na si sahihi kwake,, sasa ili kuepukana na mambo hayo yote ipo misinngi ya kuifahamu kabla hujaanza biashara, misingi hiyo ni ipi twende pa1....- ENEO LA KUFANYIA BIASHARA. katika biashara yeyote ile hili ni jambo muhimu sana la kulizigatia kabla yakuianza biashara,..Hapa utaangalia mazigira yatakayo endana na aina ya biashara unayoifaya... Mfano unataka ufungue Biasharaya ya stationary muhimu kuzigatia maeneo yaliopo kalibu na mashule , ofisi zozote za kijamiia ama kwenye mzunguko mkubwa wa watu na wanafunzi. Hapo ndipo biashara yako itakavyokweda vile inavyotakiwa na kuiona faida inayostahiki........
TAFUTA ENEO ZURI KWA BIASHARA - WATEJA .. Hapa ni lazima wewe mfanya biashara kuangalia upatikanaji wa wateja wako kulingana na aina ya biashara unayoifanya katika eneo husika, inatakiwa ujipe asilima zinazorizisha ambapo utakua unauhakika wa kuwapata wateja wanaotosheleza, hapa utaangalia kama biashara yako ni ya uuzaji wa vitabu basi wateja wako wengi watakua wanafunzi , wafanyakazi na wale watumiao vitabu hivyo kulingana na matumizi yao mbalimbali, Hivyo basi swala la kujua wateja wako ni muhimu katika aina yeyote ya biashara utakayo ifanya..
TAMBUA WATEJA WAKO - BIDHAA.. Katika biashara ni muhimu kuwa na bidhaa za kutosha zinazoweza kutatua matatizo ya wateja wako katika eneo uliloweka biashara yako, hapo ni muhimu kwa wewe mfanya biashara kutambua ni aina gani ya bidhaa zinazopendwa zaidi na wateja wako, kuwa na desturi ya kudadisi vitu vinavyopendwa zaidi na uviweke kwenye biashara yako ikizingatia na biashara unayoifanya kulingana na eneo ulilopohapo. Wateja watakua na uhakika wa huduma unazozitoa..Muhimu kuwa na bidhaa za kutosha ili kukuza biashara yako. Kwakunya hivyo utakua unauhakika wa kuwapata wateja wengi zaid...
KUWA NA BIDHAA ZA KUTOSHA - MATANGAZO. Hili ni jambo la mwisho la kulifahamu kabla ujaanza biashara yaani utaitangaza vipi biashara yako.. Kunakamsemo kanasema "Biashara matangazo", msemo huu unaukweli wa asilimia zote mia moja. hukuna biashara utakayoiendesha vizuri inavyotakiwa kama usipotagaza biashara hiyo vile inavyotakiwa, nilazima watu wapate taarifa zinazojitosheleza ili wawe na ufahamu wakutosha kuhusu bidhaa zinazopatikana kwenye biashara yako. Matangazo yako ya aina nyingi sana inategemea na biashara unayoifanya, mfano unaweza kuandaa mabango, vipeperushi au kwakupitia mitandao mbalimbali ya kijamii ama hata kama mfuko wako uko vizuri unaweza kutangaza biashara yako kwenye vyombo mbalimbali vya habari, hii itakusaidia kuweza kupata wateja wengi zaidi kwenye biashara yako na kuweza kufanya biashara yako kukua zaidi.....TANGAZA BIASHARA YAKO
- NB ........Usifanye jambo lolote kwakua umeona fulani kalifanya,.. Muhimu ni kuzingatia mambo ya msingi ya kulifanya jambo hilo, BIASHARA utaiona ni nzuri ikiwa utaona faida ile uliyoikusudia lakini inakuja kuwa chungu pale unapofikia hatua ya kuwa kila utakachokifanya matokeo yake ni kuvuna hasara.... FANYA JAMBO UKIWA UNA JUA NI NINI UNACHOKIFANYA ....... Asante kwakuwa pa1 na mimi, tukutane tena kesho nikiwaletea mada nyingine nzuri zitakazo kujenga na kukuelimisha........Mwanaharakatu LIUMA AHMED ...0719260451...................................................
Subscribe to:
Posts (Atom)